Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba Yaitungua Dodoma Jiji, Morrison na Kagere WatupiaMABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba, leo Februari 4,wamefanikiwa kushinda mchezo wao ambao ulikuwa ni kiporo, dhidi ya Dodoma Jiji baada ya kuifunga kwa magoli 2-1, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Simba walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Meddie Kagere dakika ya 27, alifunga kwa kichwa akipokea pasi murua kutoka kwa Bernard Morrison.


Goli hilo halikudumu baada ya Dodoma Jiji kusawazisha dakika ya 36 kupitia kwa Mkandala na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1.Morrison ndiye alikuwa shujaa wa Simba baada ya kufunga goli la pili kwa mkawaju mkali dakika ya 66 na kuihakikishia Simba kuvuna alama tatu muhimu.


Simba imefikisha pointi 38, baada kucheza michezo 16, Yanga inaongoza kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 44 baada ya kushuka dimbani mara 18.

Simba inatarajiwa kucheza na matajiri wa Jiji la Dar, Azam Fc siku ya jumapili Februari 7 kwenye uwanja wa Mkapa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments