Straika Yanga Amvaa Kagere Simba



STRAIKA wa Yanga, Mbukinabe, Yacouba Songne ameibuka na kubainisha wazi kuwa atapambana mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kuhakikisha anafunga mabao mengi kwa ajili ya kutwaa tuzo ya mfungaji bora.

Straika huyo ameongeza kuwa anataka kufanya hivyo kwa ajili ya kutwaa tuzo hiyo na kuisaidia timu yake kushinda michezo yao.


Mbukinabe huyo anaipigia hesabu tuzo hiyo ya ufungaji bora ambayo kwa msimu uliopita ilichukuliwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere aliye Simba baada ya kufunga mabao 22.

Yacouba hadi sasa katika Ligi Kuu Bara amefunga mabao manne akiwa nyuma ya kinara wa ufungaji John Bocco na Kagere ambao kila mmoja ana nane.

Straika huyo amelieleza Championi Jumatatu, kuwa kutwaa ufungaji bora ni ndoto ya kila mshambuliaji na kwa upande wake atajitahidi afunge zaidi kwa ajili ya kuichukua.

“Kila mshambuliaji ana ndoto na suala hilo hali ambayo ipo kwangu pia.“Nitakachofanya ni kufunga mabao mengi kwa ajili ya kujiweka katika orodha hiyo lakini pia kuisaidia timu iweze kufanya vizuri.


“Naamini Mungu atanisaidia katika suala hilo na mimi nitafanya vile ambavyo ninaweza,” alimaliza Mbukinabe huyo.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad