Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Takukuru waanza kuichunguza Temeke


Siku moja baada ya Rais John Magufuli kuiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mkopo uliochukuliwa na halmashauri ya Temeke, taasisi hiyo imeanza kazi hiyo.


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Brigedia Jenerali John Mbungo amesema maofisa wa taasisi hiyo wameanza kulifanyia kazi suala hilo.“Tumepokea maelekezo na tayari watu wapo kazini wameanza kupitia nyaraka zote zinazohusu mkopo huo kwa halmashauri na taasisi ya fedha ulikochukuliwa mkopo.“Ni mapema mno kusema tumefikia wapi ila kazi inaendelea, baada ya muda tutatoa taarifa ni kitu gani tumebaini. Kwa kifupi tumepokea maelekezo,” amesema Brigedia Jenarali Mbungo.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments