Tambwe: Sijalipwa fedha zangu na yanga

 LICHA ya Uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hersi Said ambaye ni Injinia akiwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM kukabidhiwa hesabu za mkwanja wa timu hiyo inazodaiwa na Amissi Tambwe bado hajalipwa.
Staa huyo wa Burundi aliyekipiga ndani ya Yanga amesema kuwa bado hajalipwa fedha zake ambazo ni milioni 41 baada ya kufungua kesi FIfa kwa kile alichoeleza kuwa hakulipwa stahiki zake pamoja na fedha za usajili.

Fifa iliiamuru Yanga kulipa mkwanja huo kwa Tambwe ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya posho na mshahara wake.

"Tumekamilisha kuwasilisha hesabu kwa mabosi ila mpaka sasa hakuna ujumbe niliopata kwamba fedha zimeingia ama na sielewi Yanga wamekwama wapi?.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE