Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tanzia: Mbunge na Waziri wa Zamani Seif Khatib Afariki Dunia

 


MWENYEKITI wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt. Mohammed Seif Khatib, amefariki dunia leo asubuhi Jumatatu Februari 15, 2021.

 

Mwanasiasa huyo mkongwe, amewahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, Mbunge wa Uzini vipindi kadhaa, waziri wa wizara mbalimbali katika Serikali ya Muungano.

 

Khatib ambaye bado chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi, pia alikuwa mshairi, na mwandishi aliyechapisha vitabu kadhaa.

 

Pia amefanya kazi kama Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Kwa upande wa michezo amewahi kuwa mchezaji wa soka Kikwajuni Sports Club na timu ya Taifa ya Zanzibar.

 

Katika burudani Khatibu alikuwa mwimbaji wa taarab na kwenye biashara pia alikuwa mmiliki wa kituo cha Radio ya Zenj FM.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments