Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tanzia: Waziri Sonyo Afariki Dunia

MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi, Waziri Sonyo amefariki dunia jana saa 3 usiku Feb 23, 2021 baada ya kutoka kuangalia mechi ya Simba na Al Ahly.

 

Sonyo aliyetamba zaidi na bendi za Chuchu Sound, TOT, African Revolution – Tam Tam na Victoria Sound amefia Kibaha ambako ndipo alipkuwa akiishi.
 
Mazishi ya Sonyo aliyewahi pia kuitumikia Double M Sound, yanatarajiwa kufanyika Kibaha leo Jumatano.

Moja ya ‘muhuri’ mkubwa aliouacha Sonyo katika muziki wa dansi ni wimbo wake “Masimango” alioutunga mwaka 2002 akiwa na TOT wana Achimenengule”.

Inatajwa kuwa bendi aliyokuwa akiifanyika kazi hivi karibuni ni Kitesh Band yenye maskani yake Kibaha.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments