Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Timu ya Namungo Yatinga Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Kinyonge

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


KIKOSI cha klabu ya Namungo leo kimefanikiwa kutinga katika hatua ya Makundi ya kombe la Shirikisho Afrika, licha ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Clube Desportivo 1ยบ de Agosto ya Angola.


Namungo wamefanikiwa kutinga hatua hiyo kwa matokeo ya jumla ya ushindi wa mabao 7-5, kufuatia ushindi wa mabao 6-2 walioupata Namungo katika mchezo wa kwanza uliopigwa Februari 21, mwaka huu.


Namungo sasa inajiunga na timu za Raja Club Athletic ya Morocco, Pyramid FC ya Misri na Nkana FC ya Zambia kukamilisha timu nne za kundi D la michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments