Unaambiwa Ndoa ya Kajala, Harmonize Yanukia

 


Siku zote wanasema kuwa lisemwalo lipo kama halipo basi litakuja! hivi ndivyo ilivyo kwenye uhusiano tata kati ya msanii wa Bongo Muvi, Kajala Masanja na msanii wa kizazi kipya cha Bongo fleva, Rajabu Abdulkahari ‘Harmonize’ ambao hivi karibuni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii wanazungumzia kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi.

Chanzo chetu makini, kinasema kitendo cha Harmonize kuamua kuweka picha ya Kajala, kwenye Instagram yake kama ‘profaili’ na hata kwenye mtandao wa ‘Whatsap’ akionyesha wazi yuko kwenye mapenzi na Kajala, ni ishara tosha ya kuwa watu hao wameshafika mbali kwenye uhusiano wako wa kimapenzi.

“Unajua watu hawajui wanamuona kama Harmonize, anakurupuka lakini wale watu wako muda mrefu na ukweli ni kwamba wanapenda sana hivyo inawezekana watu watamtukana lakini hawajui yaliyopo nyuma ya panzia” alisema mpashaji huyo.

Akiliendea kuzungumza chanzo hicho kilisema kuwa watu wakiwa wanaendelea kummbeza Harmonize, watakuja kusikia watu wanakaribia hata kufunga ndoa kwakuwa kuna upendo wa kweli kati yao na sio unafiki hata chembe lakini wengine wanaona kama ni utani.

“Unajua Harmonize, atawashangaza watu sana na hakuna hata mmoja ataamini kitakachotokea lakini ukweli ni kwamba Harmonize, yuko kwenye mapenzi ya kweli kabisa na Kajala, na watu wakiendelea kushangaa wataona mjamaa anachukua jumla” alisema mpashaji huyo.


Baada ya kupata ubuyu huo gazeti hili lilianza kumtafuta Kajala, na lilipomuuliza kuhusu kuchukuliwa jumla na msanii huyo wa Bongo Fleva, alisema kuwa anashangaa sana watu wengi wanakubali haraka mambo ya kwenye mitandao bila kuangalia muhusika anasemaje au analichukulije jambo hilo.“


Hii habari ishanichosha sana kwenye masikio yangu kwakuwa ni vitu ambavyo havina msingi, kama ni kweli basi kuna haja gani ya kusumbuka kichwa kwa sababu ukweli utawekwa wazi tu.“


DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Kama tuko kwenye uhusiano itajulikana maana hatuwezi kuficha mpaka mwisho kwa hiyo wanaoamini hivyo wasubiri wataona” alisema Kajala nakuomba atafutwe Harmonize, kwa sababu yeye ndio anaweka vitu hivyo.Gazeti hili lilimtafuta Harmonize kwa njia ya simu hakuweza kupatikana kwa wakati muafaka.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE