Unadhani Lulu Anatakiwa Kumfanyia nini Mama Kanumba ili Wote Waishi kwa Amani na Furaha?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Kwa mtazamo wako je ni sahihi au sio sahihi baadhi ya waandishi kuendelea kumfuata Mama Kanumba kumhoji kuhusu kifo cha Kanumba ilihali Lulu alishahukumiwa kutumikia kifungo na kutoka kwa kwa mujibu wa taratibu za kiserikali?


Kwa mtazamo wako je Lulu hajutii au kuumizwa na tukio hilo la kifo cha Kanumba?


Lulu na Mama yake walijaribu kuwa karibu na Mama Kanumba watu waliona mapichapicha yao Hadi videos wakiwa pamoja kwa furaha Kisha kufarakana



Kuna nyakati Mama Kanumba takribani Mara mbili alisema kasemehe na kumuachia Mungu lakini baadaye anaibuka tena kuonesha hajasamehe


Tunaambiwa Mama Kanumba alipata pole ya pesa nyingi Kisha kununua nyumba hapa dar, na kampuni ya Kanumba ilikuwa bado inafanya kazi na aliacha vifaa, je Mama Kanumba aliviuza au Kama anavyo imeshindikana kukodisha


tunajua sote aliyefariki hawezi kurudi Tena, Mama Kanumba pia alimpoteza Seth


Lakini kwa mtazamo wako wewe unadhani kipi kifanyike ili kuyamaliza Mama Kanumba akubali yaliyotokea kuwa yashatokea , aikubali hali Kama wazazi wengine ambao wamefiwa na watoto kwa namna Kama ya Kanumba


Unadhani Lulu anatakiwa kumfanyia nini Mama Kanumba ili wote waishi kwa amani na furaha?

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MIYE BINAFSI KWANZA NAONA MAMA KANUMBA NDIO ANAPASWA KUMUOMBA LULU MSAMAHA KWANI ALIKUWA NI MTOTO WAKATI WA TUKIO, NA KANUMBA NDIO ALIKUWA NA MAKOSA KWA KUTEMBEA NA MTOTO MDOGO WAKATI YEYE NI MTU MZIMA,

    HIVYO LULU HAPASWI KABISA KULAUMIWA NA MAMA KANUMBA!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad