Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

USHAURI WA DAKTARI: Je, tendo la ndoa linaweza kusababisha kifo ghafla?Nilipokea swali kutoka kwa msomaji mmoja aliyeniuliza endapo tendo la ndoa linaweza kusababisho kifo cha ghafla? Nadhani nimepokea swali hili kutokana na matukio yaliyoripotiwa hivi karibuni ya wapenzi kufia katika nyumba za wageni.


Ni kweli shughuli ya tendo la ndoa inaweza kusababisha kifo cha ghafla kama ikitokea hitilafu katika moyo na zaidi imeonekana kuwapata wanaume kuliko wanawake.


Imewahi kufanyiwa utafiti na kubainika tendo hilo linaweza kusababisha moyo kusimama ghafla au kupata shambulizi hatimaye kifo endapo hatua za huduma za dharula zisipochukuliwa.


Inaonyesha kuwa katika idadi ya vifo 4,557 vilivyotokana na moyo kusimama ghafla wakati wa tendo na saa moja baada ya tendo ni 34 tu vilibainika kuchochewa na tendo lenyewe. Katika vifo hivyo, 32 walikuwa ni wanaume wenye umri mkubwa.


Utafiti huu ulikuwa wa awali kabisa, ulifanyika nchini Uingereza na taasisi ya moyo ya Cedars-Sinai chini ya mwanasayansi wa tiba, Sumeet Chughna na matokeo yake yaliwekwa bayana Novemba 12, 2013. Kazi kubwa ya Chughna na jopo lake ilikuwa kuchunguza kama kujamiiana ni kisababishi cha moyo kusimama.


Moyo kusimama ghafla hutokea mara baada ya misuli ya ogani hiyo kupata hitilafu na ghafla kusimama kutoa mapigo ili kusukuma damu.


Hii husababisha muathirika kupoteza fahamu na kushindwa kupumua na kufariki ghafla au baada ya muda mfupi.


Wakati shambulizi la moyo kitabibu hujulikana kama heart attack, ni tatizo la moyo kukosa lishe ya damu aidha kutokana na matatizo kadhaa ya mishipa ya damu ikiwamo kuziba.


Cardiac Arrest na Heart Attack ndiyo matatizo ya moyo yanayochangia mara kwa mara kutokea vifo vya ghafla.


Katika utafiti uliofanywa na Dk Chughna ulibaini kujamiiana kunaweza kusababisha moyo kusimama ghafla na kufariki, ingawa tatizo hilo ni nadra kutokea.


Utafiti huu ulibaini kuwa tatizo hilo linawapata zaidi wanaume wenye umri mkubwa hasa wazee.


Watu ambao wako katika hatari ya kupata tatizo hili ni pamoja na wazee, wanaoishi na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, waliowahi kupata shambulizi la moyo, kiharusi na kisukari.


Vilevile watu wanaotumia dawa kama za kuongeza nguvu za kiume, vichochezi na dawa za kuifanya damu isigande au wenye matatizo ya damu kuganda.


Tatizo hili la kufariki wakati au mara baada ya kushiriki tendo la ndoa linawapata zaidi wanaume sababu ikidhaniwa na mienendo na mitindo ya kimaisha, kibailojia na kijenetiki.


Kutokana na tendo la ndoa kuleta msisimko wa kipekee katika mfumo wa fahamu na mabadiliko katika mfumo wa damu na moyo na vichochezi husababisha mabadiliko kadhaa ya kimwili.


Mabadiliko hayo ni pamoja na kasi ya mapigo ya moyo kuongezeka, mishipa ya damu kutanuka, kasi ya upumuaji huwa juu na mwili hutumia nguvu nyingi kwa ajili ya tendo hilo.


Na mara baada ya wenza kufika kileleni hufuatiwa na hali ya mwili kupoa pamoja na mchoko hii ni kutokana na mwili kutumia nguvu nyingi kutenda na kupokea misisimko hiyo.


Mwananchi

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments