Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Ushosti wa Tanasha, Mobeto Wafika Ukingoni

KIMEWAKA? Taarifa ikufikie kwamba, ule ushosti wa wazazi wenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamisa Mobeto na Tanasha Donna, unadaiwa kutumbukia nyongo na kuwa shakani.

 

Ghafla tu, habari za ndani zinadai kwamba, Mobeto na Tanasha wamechuniana, hasa kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii ambapo wamezoeleka kuchati na kujibizana wanapoposti vitu vyao.

 

Pamoja na kwamba, wawili hao kila mmoja ni mfuasi wa mwenzake kwenye mitandao ya kijamii, lakini mara tu baada ya Tanasha kutua kwa Diamond au Mondi hivi karibuni akiambatana na mwanaye Naseeb Junior, timu ya Mobeto imemaindi na kufunga milango na imeweka mgomo wa kukomenti kwenye ukurasa wa Tanasha.

 

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kwamba, zimepita siku kadhaa tangu Tanasha alipotua nyumbani kwa Mondi na ni idadi hiyohiyo ya siku ambazo hakuna aliyekomenti kwenye ukurasa wa mwingine.Inafahamika kwamba, wanawake ambao wameshea mwanaume mmoja ni vigumu mno kuiva kwenye chungu kimoja na hicho ndicho kinachotokea.Hii ni kwa sababu kila mmoja humuonea mwenzake wivu kwa kuwa kila mmoja hutamani kuwa yeye ndiye yeye kwa mwanaume huyo.

 

Lakini awali, hali haikuwa hivyo kati ya Mobeto na Tanasha ambapo walionekana kupeana kampani na kuwa mashosti wa karibu huku wakionesha kupeana sapoti ya nguvu kwenye kazi zao za kisanaa.Ukaribu wa Mobeto na Tanasha ulikuwa gumzo kutokana na kila mmoja kuzaa na Mondi hasa pale Mobeto alipovalishwa na Tanasha alipokuwa kishuti video ya wimbo wake.

 

Hata hivyo, mara tu baada ya Tanasha kutua kwa Mondi, hali imebadilika.Katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA kuhusu kuharibika kwa ushosti wake na Tanasha, Mobeto anasema kuwa, asingependa kuzungumza lolote kwa sasa labda atafutwe siku kadhaa mbele.

 

“Nisingependa niseme lolote, naomba unitafute siku nyingine mbeleni…” Anasema Mobeto kwa kifupi.Kwa upande wake Tanasha anasema; “Hamisa (Mobeto) sijui nimuite mzazi mwenzangu…hapana siyo mzazi mwenzangu…mimi na Hamisa ni marafiki na hatuna tatizo lolote.”

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments