Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wanne Mbaroni kwa Kuzusha Vifo vya CoronaJESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu wanne waliokamatwa ndani ya Mkoa huo wakituhumiwa kutumia mitandao ya kijamii kueneza uvumi wa vifo vya Watu wakidai wamekufa kwa Corona na kutia hofu wanachi.

 

 

Kamanda wa Polisi Pwani Wankyo Nyigesa amesema; “Watuhumiwa hawa wanne tuliowakamata Pwani na wengine ambao tunaendelea kuwatafuta wanasambaza taarifa za uvumi za vifo vya Watu wakidai wamekufa kwa Corona na pia wanapendekeza majina ya Viongozi wa Serikali ambao walitamani wafe haraka kwa Corona.

 

 

” Na wengine ambao tunawatafuta, licha ya kueneza uvumi wa vifo vya Watu wakidai wamekufa kwa Corona,pia wanatia hofu Mitandaoni kwa kudai Watanzania walio wengi watakufa kwasababu Serikali haichukui tahadhari dhidi ya Wananchi wake.”

 

 

“Zaidi sana watuhumiwa hawa wanaendelea kutaja baadhi ya Viongozi Wakuu Serikalini ambao wao wanatamani wafe kwa Corona haraka sana. Wanasema Serikali haijachukua tahadhari kwahiyo Watanzania wengi watakufa kwa Corona,” amesema Nyigesa.

 

 

Amewataja waliokamatwa kuwa ni Frank Nyange (47), Moses Goodluck (34), Mohammed Abdallah Lutambi (45) na Bumija Moses (55) ambao ni Viongozi wa CHADEMA.

 

 

RPC Nyigesa amesema kama Mwananchi au Familia imefiwa, mwenye jukumu kutangaza kifo ni Wanafamilia. Aidha, kama ni Kiongozi Mamlaka za Serikali zitatangaza na sio vinginevyo.

 

 

“Polisi Mkoani Pwani tunatoa rai kwa Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya na kujiepusha na matumizi mabaya ya Mitandao ikiwemo kutoa taarifa za uvumi kuhusu vifo vya Watu ambazo zinatia hofu Wananchi wengi,” amesema RPC Nyigesa.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments