Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wastara: Mama Ulitaka Lulu Akaishi Kwenye Kaburi la Kanumba?


MSANII nguli wa Bongo Movies, Wastara Juma,ameshindwa kuvumilia na kuamua kumtolea uvivu mama wa aliyekuwa msanii namba moja wa Bongo Movies, marehemu Steven Charles Kanumba, akisema mama huyo anapaswa sasa kumuacha Lulu aendelee na maisha yake badala ya kumfuatilia kila mara na kumsemasema.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wastara amesema: “Mama Kanumba mamaa nakuita tena mama! MUNGU wetu alisema niombeni msamaha nitawasemehe sidhani kama kweli Lulu hajawahi kukuomba msamaha lakini inaonyesha kuna aina ya msamaha unaoutaka na pia hakuna kitakachobadilika kwa sababu Kanumba ameshafariki usamehe au usisamehe hatorudi tena duniani.

“Unastaajabisha kuona mpaka leo Lulu umemkalia kooni ni mbaya sana kiukweli hata kwa mwanao huko alipo unamtesa mtoto wako kaburini kwa kisasi chako, unamzuia mwanao asipate malipo kwa Mungu kwa ajili ya hasira yako unafikiria ya Mungu kweli unafikiria maandiko kweli ndani ya miaka tisa sasa lakini bado una kinyongo ni ajabu sana tena haipendezi kabisa.

“Maana na wewe ni kioo cha jamii kukaa mbele ya camera na kuongea na kuonyesha wazi una chuki za wazi na Lulu au ulitaka afe au mahakama ingemnyonga ndiyo ungeridhika na ungevuna nini labda lingetokea hilo.

“Kikubwa unachotakiwa kufanya ni kusamehe na kusahau kuhusu Lulu na usiwe unamtia mdomoni kila wakati unaojisikia wewe siyo sawa watu hawakutafsiri vizuri wanakusema vibaya na unaonekana una roho mbaya, je hii ni nzuri kwako kuonekana mbaya??

“Lakini unayataka mwenyewe kudharauliwa mama na kwa nini hasa unafanya hivi kwa sababu gani kwa sababu Lulu anaendelea na maisha yake ulitaka akaishi juu ya kaburi la Kanumba ndiyo ionekane na yeye ameumia na ameomba msamaha wa kweli?

“Unasema Lulu kasema hataki kuwa mtumwa ni kweli hataki kwa maneno yako inaonyesha unataka kumfanya mtumwa wako kwa kosa lililotokea akunyenyekee wewe na ashindwe kuendesha hata maisha yake mwenyewe ni nani angetaka kuishi hivyo mpendwa mama?  Mama nyamaza inatosha acha kuongea na usamehe ili na wewe Mungu akusamehe kwa makosa uliyowahi kufanya.” Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments