Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Watano mbaroni wakituhumiwa kwa mauaji, kujeruhi
Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo mauaji ya  wivu wa mapenzi.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Februari 24, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,  Jumanne Muliro amesema watu hao walikamatwa maeneo tofauti mkoani humo.Amesema wawili walikamatwa katika kata ya Ibisabageni Wilaya ya Sengerema mkoani wakituhumiwa kumuua  Zacharia Mussa (26) mkazi wa Mnadani Februari 21, 2021.“Inadaiwa chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi ambapo watuhumiwa hao walimjeruhi kwa kitu chenye ncha kali na baadaye akapoteza maisha,” amesema Muliro.Amesema watuhumiwa hao  bado wanahojiwa kwa kina na utaratibu wa kisheria utafuatwa ili kufikishwa mahakamani.Katika tukio la pili,  Muliro amesema wanawashikilia  watu watatu kwa tuhuma za kumjeruhi Hamidu Kamugisha (22) mkazi wa Buhongwa jijini Mwanza kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kwenye mbavu.Amesema watu hao walikamatwa Februari 22, 2021 huku chanzo  cha tukio hilo kikitajwa ni kudaiana fedha.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments