Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wimbo wa Davido "IF" Wafikisha Mauzo ya Gold Marekani, Aweka Rekodi

 


Wimbo wa Davido (IF) umefanikiwa kufikia kiwango cha mauzo ya GOLD kwa nchini Marekani, yaani umeuza nakala 500,000. Wimbo huo ambao ulitoka mwaka 2017, umemfanya Davido kufikisha jumla ya nyimbo mbili zilizofikia hatua hiyo.


Wimbo wake wa kwanza kufika hadhi ya GOLD kwa Marekani ulikuwa ni (FALL) ambao pia ulitoka mwaka 2017. Davido kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika

-

"Wimbo wangu wa pili kufika Gold, Oh Mungu wangu Ninashukuru. Nyimbo mbili pekee za Afro Beat kufika mauzo ya GOLD kwa Marekani katika historia ya muziki wa Afro Beat. Mungu ni mwema. Mengi yanakuja." ameandika Davido.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments