Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Yanga SC: Tunaanzia Tulipoishia
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetamba kuwa umejizatiti kuhakikisha kikosi chao kinauwasha moto na kupata matokeo mazuri zaidi katika michezo ya mzunguko huu wa pili kuliko ilivyokuwa mzunguko wa kwanza.

 

Yanga imekuwa na wakati mzuri msimu huu ambapo mpaka sasa wao ni vinara wa msimamo wa ligi, wakiwa wamejikusanyia pointi 44 baada ya kucheza michezo 18 na sasa wamepanga kuendeleza moto pale walipoishia awali.

 

Yanga, leo itakuwa na kibarua kizito ugenini cha kucheza dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu, mchezo wa mzunguko wa kwanza kati ya timu hizo uliisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Lamine Moro.Akizungumzia malengo yao kwenye mzunguko huu wa pili Injinia, Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM na Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga alisema: “Tumejipanga vizuri kwa ajili ya michezo yetu ya mzunguko wa pili, tunajua michezo ya mzunguko huu itakuwa migumu zaidi, lakini niwahakikishie kuwa tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri.

 

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunarejesha taji la ligi kuu msimu huu, hivyo tutahakikisha tunakusanya pointi tatu muhimu katika kila mchezo ulio mbele yetu kwa kuwa tuna kikosi kizuri ambacho kinaweza kulifanikisha hilo.”

Stori: JOEL THOMAS,Dar es Salaam


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments