Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Adakwa Akiharibu Maiti Mochwari

MHUDUMU wa zamani wa mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Iten, Kaunti ya Elgeyo-Marakwet, amekamatwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma za kuharibu miili iliyohifadhiwa hospitalini humo.

 

 

Benson Kagari ambaye ni mhudumu wa zamani wa mochari hiyo, anaripotiwa kuingia katika mochwari ya hospitali hiyo Jumatano, Oktoba 28, 2020 usiku, bila kugunduliwa na mtu yeyote.

 

 

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Taifa Leo, Waziri wa Afya katika kaunti hiyo, Isaac Kamar alisema mshukiwa aliingia katika hifadhi hiyo kupitia kwenye dirisha na kuelekea hadi eneo ambapo miili hiyo ilikuwa imehifadhiwa.

 

 

Kamar alisema mshukiwa alitimuliwa hospitalini humo kutokana na utovu wa nidhamu. “Tulipokea ripoti kwamba kulikuwa na mtu aliyeingia kwenye mochari ambapo alikuwa akiharibu miili iliyohifadhiwa na kuibadilisha ili kuwachanganya wahudumu.

 

 

“Tulifika kwa haraka na kubaini kuwa ni mhudumu wa zamani aliyefutwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu,” alisema Kamar. Kulingana na Kamar, baada ya kupokea ripoti hiyo maafisa wa afya waliingia chumbani humo kwa haraka na kumfumania mshukiwa ambapo walimkamata na baadaye walimkabidhi kwa polisi ili kuchunguzwa.

 

Inasemekana kuwa mshukiwa alitumiwa na baadhi ya watu fulani kuwaharibia jina wafanyakazi katika hospitali hiyo ili kuonekana hawako makini.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments