Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Ahsanteni Tanzania kwa ukarimu wenu – Mamelodi Sundowns
Maimba ya soka nchini Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns Football Club wamewashukuru Watanzania kwa ukarimu wao katika kipindi walichokuwa hapa nchini wakijiandaa na mchezo wao wa klabu bingwa Afrika.Mamelodi wamefanikiwa kuwafunga CR Belouizdad magoli 5 – 1 ambao ndiyo waliyokuwa wenyeji baada ya Waalgeria hao kuuomba Uongozi wa Shirikisho la Mpira nchini Tanzania TFF kuutumia uwanja wa Mkapa kama dimba lao la nyumbani hapo jana.

”Tunaondoka na magoli matano na pointi 3 lakini mioyo yetu inabakia Tanzania! 🇹🇿. Ahsanteni sana kwa ukarimu wenu!,” wameandika Mamelodi Sundowns.

Magoli ya Sundowns yalifungwa na (5′, 55′ Zwane, 48′ Shalulile, 75′ Maboe, 89′ Erasmus) wakati lile la wenyeji CR Belouizdad likifungwa na (44′ Sayoud).

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments