Baba Mzazi wa Young Killer Afunguka "Mama Yake Alishamwambia Kwamba Baba yake Ameshakufa Wakati Mimi Nipo Hai"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Baba mzazi wa msanii wa HipHop Young Killer, anayefahamika kwa jina la Mzee Msodoki ambaye amesema chanzo cha kutokuwa sawa na mwanaye huyo ni mama yake kumwambia kwamba baba yake amefariki tangu utotoni.

 

Mzee Msodoki amesema mama Young Killer aliamua kumwambia hivyo mtoto wao kwa sababu aliumizwa na kitendo cha Mzee Msodoki kuukimbia ujauzito wa msanii huyo kabla hajazaliwa na kwenda kuishi nchini Congo DR.


“Mama Young Killer nilikuwa nakaa naye jirani kule Mwanza, wakati huo nilikuwa nafanya kazi Saloon, tukawa kwenye mahusiano ambayo yalidumu kama miezi 6 na baadaye akaniambia nina ujauzito, sasa kwa wakati huo mimi nilikuwa sijajiandaa kulea na majukumu hivyo nikapata safari ya kwenda Congo nilivyorudi sikumkuta” ameeleza Mzee Msodoki 


“Nimekuja kugundua kama mtoto yupo na ameshakuwa mkubwa ila mama yake alishamwambia kwamba baba yake ameshakufa wakati mimi nipo, ndiyo maana hata yeye haamini kama mimi ndiyo baba yake kweli” ameongeza 


Mzee Msodoki amesema aliwahi kukutana na Young Killer na alimwambia kama yeye ndiyo baba yake lakini alijibiwa kwamba hana shida lakini mpaka mama yake amdhibitishie

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MIKISHAONA WATOTO WAMEKUWA MAARUFU NDIO MNAJITOKEZA AAH!! MIMI BABA YAKO MIMI BABA YAKO!!!ULIKUWA WAPI SIKU ZOTE KUMTAFUTA????????????????????? MBONA SIJAONA WATOTO MAJAMBAZI BABA ZAO WANAJITOKEZA HA HA HA!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad