google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Babu Seya Alivyopigwa Butwaa Kifo cha Magufuli | UDAKU SPECIAL

Babu Seya Alivyopigwa Butwaa Kifo cha Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




NGULI wa muziki wa Dansi Tanzania, Nguza Viking ‘Babu Seya’ amesema alipigwa na butwaa baada ya kusikia kwamba aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefariki dunia; siku ile ya Machi 17, mwaka huu.

Akizungumza na safu hii, Babu Seya alisema taarifa hiyo baada ya kuisikia usiku hakulala kabisa hadi asubuhi kwa kumuombea na kumfikiria Rais huyo.

 

Babu Seya alisema alikosa usingizi kutokana na jinsi mzee huyo alivyomtoa jela ambako ni shimo zito lililokuwa limemfunika yeye na familia yake.

 

Babu Seya anasema anamuona Magufuli kama baba yake mzazi kutokana na kumtoa jela yeye na familia yake baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.“Ni yeye ametufanya sisi kuwa nje na kuiona dunia tena, kosa yeye (Magufuli) naamini tungefia jela,” alisema Babu Seya.

 

Rais John Magufuli Desemba 9, 2017 aliwaachia huru Babu Seya na mwanaye Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela.


Nguza Viking ‘Babu Seya’.

Msamaha huo unatajwa kuwa historia na hasa kuwasamehe wafungwa wa maisha na wale wa kunyongwa ambapo kwa wa kunyongwa walioachiwa huru ni 61 na wengine walioachiwa huru kutokana na makosa mbalimbali ni 1,821 huku wengine 8,157 aliwapunguzia adhabu zao.

 

Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kuwabaka na kulawiti watoto wa shule.Mwaka 2010, rufaa yao ilisikilizwa katika Mahakama ya Rufaa na kuwaachia huru Nguza Mashine na Francis Nguza baada ya kuwaona hawana hatia katika makosa yote waliyoshitakiwa.

 

Baada ya rufaa hiyo, Babu Seya na Papii Kocha walipatikana na hatia hivyo kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

 

Tarehe 30, Oktoba mwaka 2010, Mahakama ya Rufaa iliyoketi chini ya jopo la majaji watu, likiongozwa na Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati walisikiliza hoja za pande zote kuhusu ombi la kufanyika mapitio ya uamuzi wa awali wa mahakama hiyo.

 

Mahakama ya Rufaa baada ya kufanya mapitio ikiwa imeketi chini ya majaji watatu, iliendelea kuwaona warufani hao wawili kuwa na hatia hivyo kuendelea kutumikia adhabu yao.

 

Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili wao Mabere Marando uliomba kupitiwa upya kwa uamuzi huo, ukidai kuwepo kasoro katika ushahidi uliowatia hatiani, ikiwemo kukosekana kwa mashahidi muhimu katika kesi hiyo.Majaji walisema kuwa kuna uthibitisho kuwa warufani hao wawili waliwabaka watoto wa shule ya msingi mwaka 2003.

 

Kesi hiyo iliwashtua mashabiki wa Babu Seya wa Tanzania na kanda nzima ya Afrika Mashariki.Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na mashabiki wengi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad