Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Bongo Movie kuanza safari ya Chato Jumatatu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Dar es Salaam. Wasanii wa Bongo Movie Jumatatu Machi 22, 2021 wataanza safari ya kwenda katika mazishi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli yatakayofanyika wilayani Chato Mkoa wa Geita Alhamisi Machi 25, 2021.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Machi 19, 2021 mratibu wa safari hiyo, Steven Mengere maarufu Steve Nyerere amesema wataondoka saa 12 asubuhi.

“Magufuli kwa wasanii alikuwa zaidi ya baba, alileta mapinduzi makubwa katika tasnia walau sasa tunafaidika na kazi zetu na pia usimamizi umekuwa mzuri.”

“Tuna kila sababu ya kwenda kumsindikiza katika safari yake ya mwisho hapa duniani na tayari tumeandaa gari aina ya Coaster mbili ambazo zitawabeba wasaniiwa Bongo Movie katika safari hiyo,” alisema msanii huyo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments