Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Breaking News: Bunge Lamthibitisha Mpango Kuwa Makamu wa Rais
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amethibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu wa Rais Mteule, kwa kupata kura zote 363 za ndiyo (sawa na asilimia 100) ya kura zote zilizopigwea na wabunge leo Machi 30, 2021, Bungeni jijini Dodoma.


Akitangaza matyokeo ya kura hizo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema tarehe ya kiapo cha uaminifu cha Makamu wa Rais kitafanyika mbele ya Jaji Mkuu, tarehe ambayo itapangwa baadaye.


Aidha, Ndugai amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mpango sasa ubunge wake umekoma leo baada ya kupitishwa hivyo jimbo lake la Buhingwe, mkoani Dodoma alilokuwa akiliongoza liko wazi na uchaguzi utafanyika kulijaza.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments