Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Breaking NEWS: Msafara Wa Makamu Wa Pili Wa Rais Zanzibar Wapata Ajali

 


 

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya gari lililokuwa limewabeba waandishi wa habari katika msafara wa makamu wa pili wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, kupata ajali mua mfupi uliopita visiwani Zanzibar.


Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia hivi punde, aliyefariki dunia ni Hamis Machenga, afisa anayeshughulikia masuala ya habari katika ofisi ya makamu wa pili wa rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdallah.


Waandishi wengine wapatao wanne pamoja na dereva wa gari lililopata ajali, wamekimbizwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wanakoendelea kupatiwa matibabu.


Chanzo cha ajali hiyo, kinaelezwa kuwa ni baada ya gari lililokuwa likiendeshwa na raia mmoja wa kigeni, kuingilia msafara huo na kuligonga gari lililokuwa limewabeba waandishi na kusababisha lipinduke.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments