Corona inaua zaidi wanaume kuliko wanawake Afrika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa virusi vya corona vinasababisha vifo kwa wanaume wengi zaidi barani Afrika kuliko wanawake ambao kwa sehemu kubwa waandamwa na uwezekano wa kupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi kuliko Covid-19.


Utafiti uliofanywa kwenye nchini 28 za Afrika, ikiwemo Guinea, Mauritius na Uganda umeonesha kwa wastani idadi ya wanawake waliopata maambukizi au kufa kwa corona ni ndogo ikilinganishwa na wanaume.


Takwimu zilizokusanywa zinaonesha kwa wastani asilimia 41 ya wanawake barani Afrika ndiyo wamekumbwa na janga la corona lakini idadi hiyo inatofautiana miongoni mwa mataifa.


Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika Matshidiso Moeti amesema kwa wanawake janga la covid-19 limesababisha ukosefu wa huduma za uzazi na wengi wanaweza kufariki kwa sababu hiyo kuliko matatizo yanayotokana na virusi vya corona.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad