COSOTA Yatoa Angalizo kwa Televisheni zinazonunua kazi za Filamu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Mwanasheria wa COSOTA Lupakisyo Mwambinga akiendesha kikao cha usuluhishi wa mgogoro kati ya Mmiliki  wa Tamthilia  ya Likuru the Village Elders Bw. Charles Ayuko (hayupo pichani) iliyoandaliwa na Kampuni ya Ladha ya Mtaa kutoka Kenya na Meneja wa Vipindi wa Televisheni ya Plus TV zamani Clouds Plus Tv Isaya Kandonga, leo Machi 06, 2021 Jijini Dar es Salaam, baada  ya kituo hicho cha televisheni ya Plus Tv kurusha Tamthilia hiyo bila kupata idhini ya miliki huyo na hii ni kutokana na kununua kazi hiyo kutoka kwa wakala tapeli na kuirusha bila kufanya uhakiki wa umiliki wa kazi hiyo.


Mmiliki  wa Tamthilia  ya Likuru the Village Elders Bw. Charles Ayuko (hayupo pichani) iliyoandaliwa na Kampuni ya Ladha ya Mtaa kutoka Kenya akitoa shukrani kwa uongozi wa COSOTA kwa namna walivyomsaidia kupata haki yake kwa maongezi ya amani baina ya pande zote mbili, baada ya Tamthilia yake kurushwa na Televisheni ya Plus Tv zamani Clouds Plus pasipo kuwa na makubaliano nae leo Machi 06, 2021, mara baada kikao cha usuluhishi kilichoendeshwa na COSOTA katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.


Meneja wa Vipindi Televisheni ya Plus TV zamani Clouds Plus Tv Isaya Kandonga, leo Machi 06, 2021 Jijini Dar es Salaam akikiri kurusha Tamthilia ya Likuru the Village Elders bila kuhakiki vyema umiliki wa kazi hiyo baada ya kuuziwa na wakala tapeli aliyedai ni mmiliki wa kazi hiyo ambapo ameeleza uongozi wa Plus umeridhia kulipa milioni sita pamoja na gharama nyingine kwa mmlikili wa kazi hiyo Bw. Charles Ayuko kutoka nchini Kenya katika kikao cha usuluhishi wa kesi hiyo uliyoendeshwa na COSOTA katika ofisi zao.


Mwanasheria wa COSOTA Lupakisyo Mwambinga akiendesha kikao cha usuluhishi wa mgogoro kati ya Mmiliki  wa Tamthilia  ya Likuru the Village Elders Bw. Charles Ayuko (hayupo pichani) iliyoandaliwa na Kampuni ya Ladha ya Mtaa kutoka Kenya &t;/span>na Meneja wa Vipindi wa Televisheni ya Plus TV zamani Clouds Plus Tv Isaya Kandonga, leo Machi 06, 2021 Jijini Dar es Salaam, baada  ya kituo hicho cha televisheni ya Plus Tv kurusha Tamthilia hiyo bila kupata idhini ya miliki huyo na hii ni kutokana na kununua kazi hiyo kutoka kwa wakala tapeli na kuirusha bila kufanya uhakiki wa umiliki wa kazi hiyo.

 





 

Na Anitha Jonas - COSOTA, Dar es Salaam.


 Uongozi wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) umetoa wito kwa vituo vya Televisheni  vinavyonunua Tamthilia na Filamu kuhakikisha wanahakiki Umiliki wa kazi hizo COSOTA kabla ya kuzirusha.

 Wito huo umetolewa leo Machi 06, 2021 Jijini Dar es Salaam na Mwanasheria wa COSOTA  Bw.Lupakisyo Mwambinga katika kikao cha kutatua mgogoro  kati ya  Muandaaji wa Tamthilia Likuru the Village Elders iliyoandaliwa na  Kampuni ya Ladha ya Mtaa ya nchini Kenya, ambapo tamthilia hiyo ilirushwa na televisheni ya Clouds Plus TV  hivi sasa Plus TV ya nchini Tanzania ilirusha  kazi hiyo bila ya kuhakiki Umiliki baada ya kuinunua kazi hiyo kutoka wakala aliyewauzia nakujikuta wameingia katika mgogoro huo.

 "COSOTA imekuwa ikitoa huduma ya kuhakiki umiliki wa kazi zote za Sanaa na Ubunifu ikiwemo kwenye Filamu na Muziki hivyo ni vyema kila unaponunua Filamu yoyote au tamthilia ilete COSOTA tukusaidie kukagua umiliki wake kwa lengo la kuepuka migogoro na kulipa faini kubwa kutoka kwa mmiliki halali wa kazi hiyo,"alisema Mwambinga.

 Pamoja na hayo nae Mwendeshaji wa Vipindi kutoka kituo cha Plus Tv zamani Clouds Plus Tv Bw.Isaya Kandonga  ametoa angalizo kwa Wafanyabiashara kuwa makini wanaponunua kazi hizo kutoka kwa mawakala mbalimbali.

 "Pongezi kwa uongozi wa COSOTA  kwa namna walivyosimamia mgogoro huu  na kuhakikisha tunamaliza kesi hii kwa maridhiano mazuri na kupitia kesi hii uongozi wa Plus Tv umejifunza kwa sasa kwa kila Filamu au Tamthilia tunayonunua tutahakikisha tunaiwasilisha COSOTA kwa ajili ya kuhakiki umiliki wake," Bw.Kandonga.

 Katika kikao hicho Bw.Kandonga alieleza kuwa uongozi umeridhia kulipa kiasi cha Shilingi Milioni Sita, pamoja na gharama nyingine  kwa mmiliki wa kazi hiyo Bw. Ayuko ikiwa ni fidia ya kurusha kazi hiyo bila ya kuingia makubaliano na mmiliki huyo.

 Kwa upande wa Muandaaji wa Tamthilia hiyo ya  Likuru the Village Elders kutoka Kenya alipongeza na kushukuru uongozi wa COSOTA kwa namna walivyomsadia kupata haki yake.

Halikadhalika kufuatia mashirikiano mazuri ya Taasisi ya COSOTA na nchini  nyingine,  mlalamikaji aliwasiliana na ofisi ya Hakimiliki Kenya (Kenya Copyright Board - KECOBO) na kupewa barua ya utambulisho kuja COSOTA na alipofika katika ofisi hizo Tanzania alisaidiwa vyema malalamiko yake.

 Hivyo basi COSOTA inatoa rai kwa Wasanii wote watanzania kutosita kufika katika ofisi zao kuomba msaada wa kisheria pale wanapopata changamoto yoyote ya kazi zao kutumika popote ndani na nje ya nchi bila ya kuwepo na makubaliano.

L
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad