Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Dar: Jela Miaka 30 kwa Kuiba Simu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Mahakama ya Wilaya ya Temeke imewahukumu Hemed Salum na Musa Musuni kifungo cha miaka 30 jela kutokana na kosa la kuiba simu ya Tsh. 200,000 pamoja na Tsh. 10,000 wakitumia silaha.

 

 

Walitenda kosa hilo Novemba mwaka 2019 eneo la Mikoroshini, Temeke ambapo walimpora Easter Asheli simu na fedha ambapo kabla ya kufanya hivyo walimjeruhi kwa kisu.

 

Katika maelezo yao, washtakiwa walidai baada ya kuiba simu waliiuza kwa Tsh. 80,000 na kugawana Tsh. 40,000 kisha wakakimbilia Bagamoyo.

 

Hakimu Mkazi, Anna Mpessa, amesema Mahakama imejiridhisha na ushahidi ulitolewa akieleza kosa la unyang’anyi limekuwa sugu na kupelekea Watu kupata ulemavu wa maisha na kurudisha nyuma maendeleo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments