Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Derby Ya Wanawake Yakoleza Kuelekea Siku Wanawake Duniani, Simba Queens yaichabanga Yanga Princess bao 3-0

Timu za watani wa jadi katika soka la Wanawake kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess, imechezwa jioni ya leo Ijumaa 05/03/2021 katika dimba la Uhuru Wilaya ya Temeke, Dar es salaam.

Katika mchezo huo Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa magoli 3 kwa 0 dhidi ya mahasimu wao Yanga Princess.

Magoli ya Simba yamefungwa na Nahodha Mwanahamisi Omary (30), Opah Clement  (Penati, 43) na Joel Bukuru (50).

Kwa matokea haya ya leo,  Simba Queens inashika usukani wa ligi ya wanawake kwa kuwa na Point 39 huku wakiwaacha watani wao nyuma kwa pointi moja yaani wakiwa na pointi 38.

Mtanange huo umeenda sambamba kabisa matukio yanayohusisha shughuli za Wanawake kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani kinaadhimishwa machi 08, 2021. ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Mwanamke  #ChaguaKupambana.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments