Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Dude Apata Ajali Tatu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
MSANII wa filamu Bongo Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amesema mwaka jana 2020 haukuwa mwaka mzuri kwake kwani alipata ajali tatu za kutoa uhai wake lakini anamshukuru Mungu alifanikiwa kutoka salama.

 

 

Dude amesema ajali ya kwanza ilikuwa ya gari na ilimfanya asitembee miezi mitatu ambapo alisaidiwa na mchezaji Mbwana Samatta na ajali zingine mbili alipata ndani ya mwezi mmoja wakati wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

 

“Nilipata ajali zinginge mbili ndani ya mwezi mmoja, ya kwanza nilipata wakati wa ufunguzi wa Kampeni za CCM, ya pili nilipata wakati Rais anahutubia Kampeni Kawe na zote zilikuwa za bodaboda, ajali ya pili nilipata nikiwa na majeraha ya ajali ya kwanza.

 

 

“Ajali ya pili tairi la mbele la bodaboda likapasuka, rim ikapinda tukapaa tukatua kwenye lami, mimi nikapona mwenzangu akafariki, ulikuwa mwaka mbaya sana kwangu zile zilikuwa ajali za kutoa uhai, nilimrudia Mungu kwa kusoma dua na watoto wa chuo ‘Madrasa’ na yatima,” ameongezaPost a Comment

0 Comments