Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Gomes Aja na Mikakati Mipya ya Ubingwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
KOCHA Mkuu wa Simba raia wa Ufaransa, Didier Gomes, amesema anafahamu ugumu umeongezeka wa Ligi Kuu Bara, lakini hataki iwe sababu ya kupata matokeo mabaya na badala yake wachezaji wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ili wawaondoe Yanga kileleni.

 

Simba ambayo jana ilicheza na Prisons, inapambana kuhakikisha inaishusha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na kutetea ubingwa wao.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema matokeo ya ushindi katika kila mchezo kwao ni muhimu, hivyo ni lazima vijana wake wapambane kuhakikisha wanatimiza malengo ya kubeba ubingwa wa ligi na Kombe la FA.

 

Gomes alisema kuwa ana imani kubwa na ubora wa kikosi chake ambacho kinaundwa na wachezaji wengi wenye viwango bora.“Mchezo wetu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh washambuliaji wangu walikosa umakini uliosababisha tutoke suluhu.“

 

Sitaki kuona makosa yakijirudia, tayari nimekaa na wachezaji wangu na kuwaambia nafasi moja haiwezi kujirudia mara mbili, hivyo kila nafasi tutakayoipata lazima tuitumie vizuri kwa kufunga mabao.“

 

Nafahamu ugumu wa ligi umeongezeka katika mzunguko wa pili, lakini hiyo haiwezi kutufanya tupoteze michezo yetu, kikubwa ninahitaji ushindi pekee ili tuwaondoe walio juu yetu katika msimamo,” alisema Gomes


Post a Comment

0 Comments