Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Hesabu ngumu za taifa stars, kufuzu AFCON

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Hatima ya timu ya taifa ya Tanzania taifa stars kufuzu fainali za AFCON kwa mara ya pili mfululizo itajulikana leo usiku itakapo minyana na Equatoria Guinea ugenini, ukiwa ni mchezo wa kundi J mchezo utakao chezwa majira ya Saa 4:00 Usiku.

 

Tofauti ya timu hizi kwenye msimamo wa kundi ni alama 2, Equatorial Guinea wapo juu ya Tanzania wakiwa na alama 6, wakati Tanzania wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 3 kwenye michezo 4 waliocheza mpaka hivi sasa kwenye hatua ya makundi ikiwa imesalia michezo miwili.


Hivyo usiku wa leo taifa stars inahitaji ushindi pekee ilikujihakikishia nafasi ya kufuzu kwenye fainali hizo zitakazo fanyika nchi Cameroon mwezi Januari mwaka 2022, na endapo kama Tanzia ikifungwa kwenye mchezo wa usiku wa leo basi haitakuwa na nafasi ya kufuzu kwenye fainali hizo.


Endapo kama Stars ikishinda itafikisha alama 7 na itapanda mpaka nafasi ya pili, itaishusha Equatoria Guinea ambao kwa sasa wapo kwenye nafasi hiyo. Na kama Equatoria Guinea wakishinda watafikisha alama 9 ambazo Tanzania hawawezi kuzifikia na utakuwa umesalia mchezo mmoja.


Kwenye msimamo wa kundi J’ Tunisia ndio vinara wana alama 10, na wameshafuzu kwani kwa alama hizo hawawezi kumaliza nje ya nafasi mbili za juu, hivyo ni nafasi moja ndio inayowaniwa.


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments