Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Hii ndiyo sababu ya Mama Janeth kutofika Zanzibar

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kuwa kutokana na hali ya huzuni aliyokuwa nayo mjane wa Hayati Dkt. Magufuli, Mama Janeth Magufuli, walimuomba asishiriki shughuli ya kuaga mwili wa mume wake inayofanyika Zanzibar hii leo na badala yake atangulie Mwanza watamkuta huko.

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 23, 2021, kwenye Uwanja wa Amani visiwani Zanzibar, wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, na kuwaomba Watanzania pamoja na viongozi wa serikali kuendelea kumpa pole Mama Janeth.


"Tuendelee kutoa pole kwa mke wa marehemu ambaye hakumudu kufika leo, tulimuomba kwa kweli apumzike kwa sababu kuanzia jana ana huzuni sana kwahiyo tukamsihi atangulie Mwanza tutamkuta huko," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.


Awali akizungumza na wananchi wa Zanzibar waliojitokeza kuaga mwili huo amesema kuwa mwili huo pia hii leo utalala Ikulu ya Zanzibar, "Leo mtapata fursa ya kupita mmoja mmoja mbele ya jeneza na kumuaga, tunaamini kwa idadi hii haiwezi kuchukua masaa mengi lakini tutakuwa hapa hata kama tutamaliza saa 6 usiku ili mradi kila mmoja amalize kiu ya kumuaga kiongozi wetu".

Post a Comment

0 Comments