Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Hukumu ya kesi ya Shamim Mwasha na mumewe machi 31

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


MAHAKAMA Kuu kitengo cha Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imepanga kutoa hukumu dhidi ya mfanyabiashara, Abdul Nsembo (45) maarufu kama Abdulkandida na mkewe, Shamim Mwasha (41) Jumatano Machi 31, Mwaka huu.
Hukumu hiyo itatolewa baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kumaliza kutoa ushahidi wao.

Upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi sita na vielelezo NANE huku upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi watatu.

Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog ya 8020 na mumewe Nsembo, wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini gramu 439.70, wanadaiwa kutenda tukio hilo Mei mosi 2019 huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Elinaza Luvanda.

Post a Comment

0 Comments