Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Jembe Jipya Larudisha Tabasamu Yanga SC

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


KUREJEA kwa jembe jipya la Yanga ndani ya kikosi hicho, unaweza kusema tabasamu la Wanayanga limerudi, hii ni baada ya timu yao kwa siku za karibuni kuonekana kuyumba kidogo.

 

Dickson Job ambaye ni beki mpya wa kati wa Yanga, alikuwa nje ya kikosi hicho kwa muda kidogo ambapo baada ya kupona majeraha yake, alipata matatizo ya kifamilia, lakini sasa ameyatatua na kurudi kambini.

 

Job ambaye hajaichezea Yanga mchezo wowote tangu atue kikosini hapo kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, kurejea kwake huenda kukaimarisha zaidi safu ya ulinzi ya timu hiyo.Akizungumza na Spoti Xtra,Job alisema: “Baada ya kumaliza changamoto za kifamilia ambazo zilinikumba hivi karibuni, natarajia kujiunga na kikosi kesho (jana) Jumamosi kwa ajili ya kujiandaa na michezo iliyo mbele yetu.

 

“Sijapata nafasi ya kuichezea Yanga mpaka sasa kutokana na changamoto mbalimbali, lakini naamini kwa kuwa kila kitu sasa kimekaa sawa, nitajitahidi kuhakikisha najituma kuisaidia timu yangu kila nitakapopata nafasi ya kucheza.”


Post a Comment

0 Comments