Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Juma Mwambusi abeba mikoba ya Cedric Kaze
Klabu ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wake Dr.Mshndo Msola imemtangaza Juma Mwambusi Kama kocha wa muda, hii ikija baada ya benchi zima la Yanga kutimuliwa hapo juzi.Mwambusi ambaye alitamba na Klabu ya Mbeya City Kama kocha mkuu na amewahi kupita Yanga, Singida United na Azam akiwa Kama kocha msaidizi anarudi kwenye Klabu hiyo ikiwa ni miezi michache tangu aondoke kwenye nafasi ya kocha msaidizi kwenye klabu hiyo.“Mwambusi ataichukua timu kwasasa wakati tunamtafuta mwalimu mwingine, na kwa bahati nzuri Mwambusi aliondoka na kuaga vizuri, na klabu ilimsaidia kupata matibabu wakati anaumwa na tokea ligi inaanza tulikuwa naye hivyo sio kwamba ana ugeni na timu”

Dr Mshindo Msola mwenyekiti wa Klabu ya Yanga ameyasema hayo akiwa anamtangaza Juma Mwambusi kama kocha wa Yanga kwa muda.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments