Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kampuni yanunua mawe yaliopakwa rangi ikidhani shaba, kesi yaunguruma mahakamani

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Kesi mahakamani ni jambo la kawaida katika ulimwengu ya biashara lakini kesi iliyofunguliwa na moja ya kampuni kubwa ya utengenezaji bidhaa imevutia nadhari isiyo ya kawaida.

getty images

Kampuni kubwa ya Uswizi ya Mercuria Energy Group, imeshitaki kampuni ya uuzaji wa shaba ya Uturuki baada ya kupokea mzigo wa kile ilichotakiwa kuwa tani 6,000 za madini ya shaba lakini ikabainika kwamba ni mawe yaliyopakwa rangi.

Sakata hiyo ilianza katikati ya mwaka wa 2020 pale kampuni moja ya kimataifa iliyo na makao yake mjini Geneva ilipotia saini makubaliano na kampuni ya Uturuki ya Bietsan Bakir katika ununuzi wa tani 10,000 za shaba ambayo haijasafishwa yenye muonekano wa kama malengelenge.

Na baada ya majadiliano mzigo huo ulisafirishwa hadi nchini China.

Katika bandari karibu na Istanbul, tani 6,000 za shaba zilipakiwa katika makontena zaidi ya 300 ambayo yangesafirishwa kwa meli nane.

Lakini kontena ya kwanza ilipowasili katika nchi ya bara Asia, ikagundulika kuwa badala ya kuwa na shaba, makontena yalikuwa yamejazwa mawe mawe yaliyopakwa rangi.

Inaaminika kwamba kabla ya kuanza safari, shaba iliyokuwa imepakiwa ilibadilishwa na kupakiwa mawe yaliyopakwa rangi.

Kesi hiyo ya ulaghai isiyo ya kawaida ilijitokeza licha ya uwepo wa usalama na udhibiti wa ukaguzi.

Kukamatwa
Sasa hivi Mercuria, moja ya kampuni kubwa za mafuta duniani inataka kufidiwa katika mahakama za Uturuki na Uingereza huko Bietsan Bakir, kwasababu ya kubadilishwa kwa mzigo na ulaghai wa bima.Shaba hiyo inadaiwa kubadilishwa kabla ya meli hiyo kitia nanga

Shaba hiyo inadaiwa kubadilishwa kabla ya meli hiyo kutia nanga
Wakati huo huo, polisi huko Uturuki wamewakamata watu kadhaa kuhusiana na sakata ya shaba feki.

“Washukiwa wanaaminika kuhusika na uhalifu kadhaa wa kupangwa dhidi ya kampuni ya Mercuria huko kizuizini,” taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imesema huku pia ikiishukuru idara inayoshughulikia Uhalifu wa Kifedha iliyopo Istanbul.

Wanaochunguza sakata hiyo wanaamini kuwa meli iliyokuwa na shaba halisi ilikaguliwa na wakaguzi ambao walifunga mizigo na kuweka muhuri kwenye makontena kuzuia ulaghai wowote.

Lakini, kampuni moja ya sheria ya Istabul ya KYB, imeelezea vyombo vya habari kuwa wahalifu hao walifungua tena makontena yenye mizigo hiyo na kubadilisha shaba hizo kwa mawe yaliopakwa rangi na kubandika vibandiko bandia ili isijulikane.

Punde tu baada ya meli kuanza safari kampuni ya Mercuria ililipa dola milioni 36 kwa awamu tano za malipo ya pole pole kama walivyokubaliana.

Ulaghai huo haukuwahi kujulikana hadi wahudumu wa meli ya kubeba mizigo walipowasili katika bandari ya China ya Lianyungang.

Uhalifu uliopangwa
“Kumetolewa ombi la kufanyika kwa uchunguzi wa uhalifu huo kati ya wanunuzi dhidi ya wauzaji na wengine wawili waliokuwa viunganishi kati ya mnunuzi na muuzaji,” Polisi nchini Uturuki imesema.

“Wizi huo umetambuliwa kama uhalifu wa kupangwa.”

Katika matukio ambapo mzigo haujawasilishwa kama ilivyo kwenye makubaliano, mfanyabiashara anaweza kumfungulia mwingine mashitaka dhidi ya sera ya bima ya mzigo.

Hata hivyo kampuni ya Mercuria iligundua kwamba ni mkataba mmoja tu kati ya saba iliyotumiwa na kampuni ya Uturuki kwa usalama wa mizigo ulikuwa wa kweli.

Mikataba mingine ilikuwa ni feki.
Bietsan Bakir, kampuni ya Uturuki ambayo iliuza madini ya shaba kwa kampuni ya Mercuria, haikujibu maombi ya kutaka kuzungumza nao kuhusiana na sakata hiyo pale shirika la habari la Reuters ilipowasiliana nayo.

Post a Comment

0 Comments