Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kigwangalla: Viongozi wangapi wa Africa tukifa tutaliliwa kama hayati Magufuli ?

J

Sisi viongozi wa Africa, ni wangapi kati yetu tukifa tutaliliwa na watu kama anavyoliliwa Rais Magufuli? Ni wangapi? Sisi viongozi wa Africa, ni nani akijitazama Kwa undani anaona watu wake wanampenda na kumthamini Kama alivyopendwa na kuthaminiwa Rais Magufuli? Nimekuwa nikiwaza na kuwazua, na nimepata muda wa kujitazama kwa kina na kuitazama njia ya mapito yangu kama Kiongozi wa umma, naiona ‘challenge’ anayotupa mpendwa wetu Dkt. Magufuli, naiona fursa ya kujifunza kwa kina zaidi juu ya namna Rais Magufuli alivyoishi na kuongoza watu wake, na hata akajiwekea hazina kubwa ya upendo kutoka kwa watu wake. Tunavyomlilia leo hii, tusherehekee na kujifunza kutokana na maisha yake! Nadhani akitazama nyuma, kama huwa wanaona, nadhani anamshukuru Mungu Kwa neema na baraka za maisha mazuri aliyoishi na kuacha alama kwenye maisha ya watu wake.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments