Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kofia Ya Magufuli Yampa Mzuka Kala

MSANII wa Bongo Fleva, Kala Jeremiah amesema kofia aliyovalishwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ itamfanya aendelee kumuona moyoni mwake.

 

Kala ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, kitendo cha kuvalishwa kofia na Rais huyo kilimfanya ashindwe kuamini kilichotokea alipokuwa akitoa burudani kwenye kampeni zilizofanyika Septemba 16, mwaka jana huko Biharamulo mkoani Kagera.

 

“Kama, msanii nikiwa nafanya kazi yangu jukwaani nilikuwa nikishangiliwa na wengi kutokana na kile nilichokuwa nikifanya, lakini sikuamini kama niliweza kumgusa mpaka Rais ambaye nilishtukia akiniita na kunivalisha kofia.

 

“Wakati mimi navalishwa kofia hiyo tayari wenzangu wengine walikuwa wamevalishwa, lakini mimi kwa upande wangu sikutegemea kama ningeweza kuvalishwa katika mazingira kama yale hivyo tukio hilo lilinipa ujasiri wa ajabu,” anasema Kala Jeremiah.

 

Akiendelea kuomboleza msiba wa Hayati Magufuli, Kala amesema Hayati Magufuli hakuwa Rais tu, bali alikuwa ni rafiki wa wasanii kwa jinsi alivyokuwa akishirikiana nasi katika mambo mbalimbali ya maisha ya kila siku.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments