Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Luis Miquissone achaguliwa kuwa Mchezaji Bora

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

LUIS Miquissone amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Simba kupitia tuzo ya Emirates Simba Fans player of the month.
Tuzo hiyo imetolewa leo Machi 17 muda mfupi baada ya uongozi wa Simba kuingia mkataba na Kampuni ya Emirates ambayo itakuwa inahusika kwenye kutoa tuzo hizo.

Baada ya kutangwazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwezi Februari, Luis amekabidhiwa tuzo na zawadi ya Shilingi milioni moja.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa tuzo hiyo ambayo imezinduliwa leo ni kwa ushirikiano na Kampuni ya Emirates Aluminium.

Kwa mwezi huu, Machi Luis pia amekuwa kwenye kiwango bora ambapo mabao yake matatu yameweza kuwa gumzo Afrika.

Bao lake mbele ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika liliweza kuchaguliwa kuwa bora na bao la usiku mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi liliipa pointi moja Simba.

Jana, Machi 16 alifungua ukurasa wa mabao mbele ya Al Merrikh wakati Simba ikishinda mabao 3-0 mchezo wa Ligi ya Mabingwa na kuifanya timu yake kusepa na pointi tatu mazima.

Post a Comment

0 Comments