Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Lulu Diva: Mbwa Wana Mapenzi Kuliko Binadamu

SEX lady kutoka katika kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amesema kuwa Mbwa wana mapenzi sana kuliko hata binadamu, hivyo watu waache kuchukulia poa hao wanyama.

 

Akichezesha taya na gazeti hili mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake alisema kuwa alishangaa jinsi watu walivyokuwa wanambeza Wema alivyopotelewa na Mbwa wake, kuwa kwanini alimlilia vile hadi kufikia hatua yakutangaza dau la Milioni 2.

 

“Hawajui ni jinsi gani yule Mbwa alikuwa anampa Wema furaha na amani ya moyo kila anaporudi nyumbani.“

 

Nyie Mbwa wana mapenzi sana kuliko hata binadamu, kwa sababu binadamu muda mwingine tuna maudhi sana lakini Mbwa ni mnyama aliyeumbwa tofauti sana, ukimfundisha na kumuelekeza yale ambayo wewe unataka basi anakufuatisha hivyohivyo.“

 

Binafsi nina Mbwa nyumbani yaani akiumwa na mimi naumwa, hivyo watu wamuache Wema mimi najua ni kiasi gani anaumia kwa sababu na mimi nina Mbwa pia, kama mtu ulizoea ukirudi nyumbani kanakumbilia saizi ukirudi hakuna kitu lazima uchanganyikiwe,” alisema Lulu

STORI; KHADIJA BAKARI NA MEMORISE RICHARD

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments