Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mabeste Awachana Wasanii Wapenda Kiki
RAPA mkali Bongo, Venance Mabeste amesema kuwa siku hizi kuna baadhi ya wasanii wa muziki wamesahau kabisa ni kitu gani mashabiki wao wanataka na kujikuta wakifanya skendo zisizokuwa na kichwa wala miguu.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu,
Mabeste alisema kwamba, asilimia kubwa ya wasanii wa muziki siku hizi wameingilia kazi ya wasanii wa Bongo Muvi yaani wanaigiza wao siku hizi kwa kiki zisizokuwa na tija kwenye jamii.

 

“Kuna baadhi ya wasanii wa muziki wamejisahau sana, wanashindwa kuelewa mashabiki wetu wanahitaji nini kutoka kwetu, wamejikuta wanaingilia kazi za wasanii wa Bongo Muvi, wanaigiza!

 

Unakuta msanii anaanza kwanza kutoa kiki kisha ndio anaachia ngoma, hii ni mbaya sana, tutoe muziki mzuri, wenye kuelimisha jamii na sio vitu vingine,” alisema Mabeste.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments