Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Magufuli azikwa Chato

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Hayati Dkt. John Magufuli, leo Machi 26, 2021, umepumzishwa katika nyumba yake ya milele kwenye makaburi ya familia yaliyopo Chato mkoani Geita.


Shughuli ya mazishi hayo imeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mke wa marehemu Mama Janeth Magufuli, marais wastaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.Mbali na hao shughuli hiyo pia imeshuhudiwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanafamilia, Mawaziri, Makatibu Wakuu, wasanii pamoja na baadhi ya wakazi wa Chato na maeneo jirani.Hayati Dkt. John Magufuli, alifikwa na mauti Machi 17, 2021, katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, kwa maradhi ya moyo na amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments