Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Majaliwa: Rais Magufuli Yuko Imara

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, leo Ijumaa, Machi 12, 2021, amewataka Watanzania wote wawapuuze wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Akizungumza mkoani Njombe, Majaliwa amesema; “Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu Watanzania wote, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.

 

“Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini? Leo Asubuhi wakati nakuja huku nimeongea nae kwa simu na ameniagiza niwaambie wana njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia,” mesema ajaliwa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments