Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Majambazi 5 Wauawa Dar, Wakutwa na Bastola

KAMANDA wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa  amesema Jeshi hilo limefanikiwa kuwaua majambazio watano na kufanikiwa kukamata bastola aina ya star ikiwa imefutwa namba  ikiwa na risasi tatu ndani ya magazine na maganda ya risasi mawili.

 

 

“Tarehe 27/02/2021 majira ya saa kumi na mbili asubuhi huko maeneo ya Kivule kwa Iranga, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia kikosi chake cha kupambana na ujambazi lilipata taarifa kuwa kuna majambazi sita waliokuwa kwenye gari namba T 836 DHF aina ya Toyota Noah.

 

 

“Baada ya kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari, walianza kufyatua risasi huku wakikimbia, katika majibizano hayo askari waliwapiga risasi majambazi watano huku mmoja akikimbia lakini pia askari mmoja alijerushiwa kwa risasi kichwani. Majambazi hao walichukuliwa miili yao na kupelekwa Hospitali kuhifadhiwa huku aliyekimbia akiendelea kusakwa.

 

Aidha, mambnosama amesema Jeshi limefanikiwa kukamata watuhumiwa 10 wa wizi wa pikipiki huku pikipiki 16 ambazo zilikuwa zimeibiwa katika maeneo mbalimbali zikikamatwa baada ya jeshi hilo kupokea taarifa kutoka kwa wahanga.

 

 

Waliokamatwa ni; Steven Paul (38) mkazi wa ulongoni A, Salum Mstaafa (28) Kigogo, Sajigwa Kaisi (25) Mongolandege A na wengine saba. Pikipiki zilizokamatwa ni; MC 967 CRT aina ya Boxer, MC 922 CSL aina ya Boxer, MC 646 CMS, aina ya Boxer na nyingine 13.

 

“Sidhani kama kuna mtu atafanya uhalifu halafu akaendelea kufaidi matunda yanayotokana na uhalifu anaoufanya, nafasi hiyo kwa Dar es Salaam hakuna. Ninawaambia vijana wangu waendelee kuchapa kazi. Yule ambaye anatumia bunduki na sisi tutahangaika naye kwa bunduki hiyohiyo, asitegemee tukija tutafanya kitu kingine,” amesema RPC Lazaro Mambosasa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments