Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Makamu Pili wa Rais Z’bar Aongoza Maelfu Kumuaga JPM Chato

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah ameongoza shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli katika uwanja wa Magufuli leo Machi 25, wilaya ya Chato Mkoani Geita.

 

Katika hotuba yake, amesema hakuna mahali ambapo Hayati Dkt. Magufuli hakuacha alama huku akitaja baadhi ya maeneo kama miundombinu ya barabara, Afya, Shule na ukusanyaji mapato kuwa ni mfano.

 

Aidha amewaomba Watanzania kuendelea kushikamana katika kujenga taifa akieleza tayari Dkt. Magufuli ameonesha njia, ameacha Taifa likiwa salama na lenye heshima kubwa.

 

“Niendelee kuwaomba Watanzania kushikamana katika kulijenga taifa, tayari mpendwa wetu ametuonyesha njia, ameliacha taifa likiwa salama na heshima kubwa, alitutoa kwenye uchumi wa chini na kutuweka kwenye uchumi wa kati”

Wakazi wa Chato watatoa heshima zao za mwisho, na gari halitozungushwa uwanjani hapo kama ilivyokuwa baadhi ya maeneo mengine.

 

Ameongeza kuwa wananchi wote walioko uwanjani hapa watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa utaratibu wa kila mmoja kupita mbele ya jeneza la Hayati Dkt. John Magufuli.


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments