Mbaroni kwa kumuua mtoto kwa kumtumbukiza kwenye jaba la maji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Jeshi la Polisi mkoani Manyara linamshikilia Tluay Shauri (46) mkazi wa kata ya Dareda kwa kosa la kumuiba ndani mtoto wa jirani yake mwenye  umri wa miezi mitatu na kumuua kwa kumtumbukiza kwenye Jaba lenye maji wakati mama wa kichanga hicho alipomlaza na kumuacha ndani wakati alipokuwa amekwenda kuchota maji kwaajili ya kufua nguo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtu huyo amekiri kutenda kitendo hicho na tayari ameshakamatwa, huku tukio hiko likihusishwa  na ugomvi baina ya familia hizo.


Kamanda kasabago  amesema mtumiwa amekiri kosa akiwa chini ya jeshi polisi na kwamba chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina yake na wazazi wa Kichanga hicho. 


Kufuatia tukio hilo wananchi wakiwemo majirani wa wazazi wa mtoto huyo wameomba hatua kali zichukuliwe kwa muhusika.


Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad