Mbaroni kwa penzi la Mwanafunzi wa shule ya msingi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Na Maridhia Ngemela  Mwanza

JESHI la Polisi mkoani Mwanza   linawashikiria watu 24 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwamo mauwaji , kuvunja ofisi za shule za msingi na kuiba  vitabu pamoja na kujihusisha na mapenzi na wanafunzi.




Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Jumanne  Muliro  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari alisema   mtuhumiwa  Japherth  Musiba amehukumiwa miaka 30 kwa  kosa la kujihusisha na mapenzi na wanafunzi  na kuwapatia mimba ambazo zinasababisha kuvunja ndoto zao.



Amesema kufanya mapenzi na mwanafunzi ni kosa kisheria kwani kubaka ,kulawiti ni vitendo ambavyo havikubariki katika jamii.





Kamanda ameongeza kuwa, Kosa la pili ni wizi wa vitabu uliofanyika katika 

ofisi za shule tatu za msingi Wilayani Kwimba  ziligundulika  kuvunjwa na kuiba vitabu 529 vya mitaala mipya vya masomo mbalimbali.



Alisema  Jeshi hilo linawashikiria walimu wa  shule tatu za Msingi ikiwamo  Igoma, Manguluma na  Bujingwa kwa kosa la kula njama za kuiba vitabu na  kutengeneza matukio ya  kufikirika ya kuvunja ili kuficha uhalisia  wa tukio hilo.



Alisema  walibaini vitabu hivyo  viliibwa na kuuzwa  kwa wafanyabiashara wa maduka ya vitabu Jijini hapa  kwani baada ya mahojiano ya kina walikili na  kuhusika na  ununuzi wa  vitabu hivyo.



" Tunawashikiria Walimu watatu ,Walinzi wanne  kwa kupokea Mali  za wizi  na mtaalamu mmoja  Mengi Muheta (43)ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Kishiri aliyekuwa anajihusisha na kufuta  alama za serikali inayosema kitabu hiki hakiuzwi,"alisema Muliro.



Hata  hivyo aliongeza kuwa  Jeshi hilo linawashikiria watu wawili  kwa tuhuma za makosa  ya mauaji  ya mtu mmoja 42  yaliyotokea  eneo la Kanyerere  kata ya Mkuyuni Wilayani Nyamagana  kwa kinachodaiwa wivu wa kimapenzi.



"Pembeni mwa mwili wa marehemu waandika ujumbe kwenye sakafu    uliosomeka kuwa mke wa mtu ni sumu kwani watuhumiwa wanafanyiwa mahojiano ya kina na upelelezi  ukikamika watafikishwa mahakamani"alisema muliro.



Kamanda ametoa wito kwa wananchi kuelekea msimu wa sikukuu ya pasaka waendelee kutoa ushirikiano kwa JESHI la Polisi na kuhimalisha usalama Katika mkoa wa Mwanza na Jeshi Hilo linajivunia kuwakamata watuhumiwa kabla ya kufanya uhalifu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad