Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mbowe Atoa Wito Huu kwa Watanzania

 


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amewaomba wanachama na wafuasi wote wa chama hicho waliondani ya nchi na nje ya nchi kuiombea familia ya Rais Magufuli, pamoja na kumuombea Mama Samia, ili aweze kusimama katika haki na kweli kwenye kuliponya Taifa.

 


Hayo ameyabainisha wakati akitoa salamu za pole za chama hicho kwa Mke wa marehemu, Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, chama na serikali na Watanzania kwa ujumla kufuatia kifo cha Rais Dkt. Magufuli, aliyefariki dunia Machi 17, 2021.


"Tunapoendelea na maombolezo tukitumie kipindi hiki kufungua ukurasa mpya wa kulirejesha Taifa kuwa moja, pia wenye mamlaka ya kisheria waheshimu na kulinda matakwa ya sheria ya katiba wakati Taifa letu likipita kipindi hiki kigumu cha mpito," imeeleza taarifa ya Mbowe.


Viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani nchini Tanzania wameendelea kutoa salamu za pole, huku wakisisitiza suala la umoja kwa Watanzania katika kipindi hiki kigumu ambacho Taifa linapitia.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments