Mbunge Amwaga Mauno Hadharani Akicheza Waah ya Mondi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mbunge wa Malindi nchini Kenya Aisha Jumwa amewachangamsha wakazi wa Matungu baada ya kunengua kiuno chake akicheza wimbo wa Diamond Platnumz wa Waah wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo ujao.

 

 

Jumwa alikuwa anampigia debe mgombea wa United Democratic Alliance (UDA) Alex Lanya ambapo alimuomba DJ kumchezea wimbo wa Diamond wa Waah ili kuwathibitishia wakazi ana kipaji cha kutingisha kiuno.

 

 

Punde wimbo huo maarufu ulipopasua anga, mwanasiasa huyo mashuhuri alianza kutingisha kiuno chake na kuwafurahisha wakazi.

 

 

Huku akiwa amezamishwa na muziki, baadhi ya wakazi walijiunga pamoja naye kwenye jukwaa na kumsaidia kuwatumbuiza wenzao ambao walishindwa kuficha furaha yao Jumwa akisakata ngoma. Uchaguzi Mdogo wa Machi 4,202.

 

 

Katika hotuba yake, mwanasiasa huyo wa Tanga Tanga aliwaomba wakazi kumpigia kura mgombea wa UDA, Lanya katika uchaguzi mdogo wa Machi 4 ambapo atamenyana na wagombea wengine 15.



 

Alisema viongozi wa Magharibi kama vile Musalia Mudavadi na Francis Atwoli wamekuwa wakiwapoteza wakazi wa eneo hilo kwa muda mrefu.

 

 

“Siku hiyo ya uchaguzi, ninawaomba nyinyi nyote mumpigie kura Lanya ili tuweze kurejea tena kuanza safari ya kuingia Ikulu pamoja,” alisema.

 

 

Kama ilivyoripotiwa awali, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iliwaidhinisha wagombea 15 kuwania kiti hicho ambacho kilisalia kufuatia kifo cha Justus Murunga.

 

 

Wagombea hao ni ikiwemo Bernard Wakoli, Gregory Atoko, Kevin Nectus, Wilberforce Lutta, Athman Wangara, Anzelimo Kongoti na Samuel Munyekenye.

 

 

Wengine ni Peter Nabulindo (ANC), David Were (ODM), Alex Lanya (UDA), Charles Kasamani (UDP), Paul Achayo (MDG) na Faida Auma wa Maendeleo Chap Chap.

Chanzo – Tuko News

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad