Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mbunge wa Muheza Tanga Aomba Radhi Kwa Wimbo Wake wa Dume Suruali


Unaukumbuka ule wimbo wa dume suruali wa Mbunge wa Jimbo la Muheza Tanga na msanii Mwana Fa, kama unaukumbuka ishu iko hivi Mwana Fa ameomba msamaha kutokana na baadhi ya lines zake alizoimba kwenye wimbo huo.

Wimbo huo ambao amemshirikisha Vanessa Mdee ulitoka mwaka 2016, sasa kupitia mtandao wa Twitter shabiki yake mmoja ali-post baadhi ya mistari inayopatikana kwenye wimbo huo kwa kuandika.

“Nihonge nanunua nini, kwanini yani? kuna kipi nisichokijua au ina TV ndani”

Baada ya muda mfupi Mwana Fa akajibu post hiyo kwa kuandika “Nilikuwa mdogo na mjeuri, mnisamehe”

Kupitia mtandao wa YouTube, video ya wimbo huo kwa sasa una watazamaji Milioni 5.3


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments