Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mchumba wa Khasshogi ataka Bin Salman aadhibiwe

Mchumba wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi amesema kwamba mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman anapaswa kuadhibiwa bila kuchelewa kutokana na kuhusika kwenye mauaji ya mchumba wake. 
Hatice Cengiz, ameyesema hayo leo katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Twitter. Cengiz, raia wa Uturuki amesema ni muhimu kwamba Bin Salman aliyeamuru mauaji hayo ya kikatili ya mtu asiye na hatia kuadhibiwa bila kuchelewa, baada ya ripoti ya kijasusi ya Marekani kubaini kuwa mwanamfalme huyo aliamuru mauaji ya Khashoggi.

 Hata hivyo, serikali ya Saudi Arabia imekanusha kuwa Bin Salman anahusika na mauaji hayo. Serikali ya Rais wa Marekani, Joe Biden siku ya Ijumaa iliweka vikwazo vya visa kwa baadhi ya raia wa Saudi Arabia wanaoaminika kuhusuika katika mauaji ya Khashoggi.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments